Posts

Showing posts from 2016
                                                             JINGA                                   Jinga!Ni jinga la moto,lifukalo likawaka,                                  Jinga!Lina utukuto,lijapozima kuwaka,                        ...
                                                                  AHA!                            Aha! Nambe sina siha,muili wangu mzima,                   Aha! Kutoona raha,ndipo aha!Nikasema,                    Aha! Sambile kwa wema,nasema kwa ndwele sii,                  Aha! Si yangu ma...
          L OWE, MOLIWA, LOKE. Lowe, Moliwa, loke, kombo nyoa penye tao, Zitangue zitanguke, suu mwiya upeleo, Ziteke zangu ziteke, ziteke zangu tekeo, Mayozi watu woyao, hunowezi name koya! Usinuwe msinuzi, suu mwiya ujileo, Pasi kombe wala mzi, wala dawa nifanyao, Ineukile simanzi, na dhiki inikuseo, Mayozi watu woyao, hunowezi name koya! Yapambanue mashaka, hayano yapembeneo, Yapate kuniepuka, yanepuke hivi leo, Uso upate kunduka, ung’are kama chiyoo, Mayozi watu woyao, hunowezi name koya!
            HISTORIA YA MUYAKA WA MUHAJI(MUYAKA BIN HAJJ) [1776-1840] Bw. Muyaka wa Muhaji alizaliwa Mombasa(Mvita,Gongwa,Kongowea,Nyali Kuu,Mzimle.)Mji wa kale ,na aliishi baina ya mwaka wa 1776 na 1840.Alikuwa shaha aliyejulikana sana katika zama zake hadi waleo kwa kutajika kuwa miongoni mwa malenga hodari na mashuhuri maarufu wa Kiswahili. Bw.Muyaka alifanya shughuli za tijara,akisafirisha malighafi za bidhaa kwa majahazi(mbiji) hadi miji mbalimbali ya ufukwe wa Afrika Mashariki mathalan visiwa vya Ngazija(Comoro islands),Bukini(Malagasy) ,Unguja(Pemba na Zanzibar) na kadhalika.Aidha alisafiri mpaka miji ya Arabuni na Bara Hindi.Mwanamtamba kule hushinda mzee wa kale.Katika kusafiri huku ,Bw.Muyaka aling'amua maarifa mengi ndiposa akawa heshi kuhusishwa mashaurini katika maswala yaliyohusiana na mji wa Gongwa. Katika aushi yake,Bw.Muyaka alimcha Mterehemezi;hakuwa na makuu na alisikizana na kuelewana na watu wengi.Alipe...
                    KONGOWEA Kongowea ja mvumo, Mvita Mji wa Kale Isokoma mititimo, na mayowe na kelele Ni ya ngao na mafumo, na mata na panga kule Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani? Gongwa ni mji muovu, viovu siukalile Hupomosha wenye nguvu, wakawa kama wawele Ikawatia kivumvu, nyoyo zikajaa tele Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani? Gongwa la Mwana Mkisi*, Mvita mji wa ole Ina waume watesi, kondo hawaiketele Wenye ghamidha na kasi, na hasira za milele Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani? Kwamba mujile na kondo, kuteta na simba wale Vumiliani vishindo, vyao msivikimbile Simba wanayo magando, makucha wayatanule Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani? Ndiswi Nyali Kuu ndiswi, ndiswi msambe tufile Ndiswi mwapigana naswi, naswi msitutawale Ni swiswi nguli ni swiswi, tuvundao miji mile Wafileo walifile, mwoleza mfu nnani? Kivumbi cha Kongowea, kivumapo ni ja ndwele Walo mbali husiki...
                          PANDA Panda, panda la mnazi, lanzalo kupapatua Panda, juu ya malazi, moyo wako weshe ngowa Panda,mti wa mapenzi, uwepushie na juwa. Panda ni wako uluwa, panda darajani panda Panda, juu ya farasi, kwa haiba na sitawa Panda, kiwango mkwasi, uukimbie ukiwa Panda, situpe viasi, wendako ukikujuwa Panda ngano na mpunga, afadhali ya viliwa Panda, wimbi wa kimanga, vipawa vya wakupewa Panda usitunde changa, tauwa mbivu tauwa Panda, mwema mshajari, wite tanzu za maua Panda ,utunde johari, mwizi asijezanguwa Panda,juu ya mimbari, ulingane sawasawa. Panda, pandio zi wazi, ukenda kwea nda kwea Panda,kwamba umkwezi, weleweo ni kukwea Panda,wala pasi ngazi shimoni nakungojea Panda,futa na mtama, upate kuvundikia Panda,juu ya mkoma, vijana wakuolea Panda, dua kwa Karima, kwa utakaso na nia.
                              ITAKAPOKUKUTANA Simba ndume na wambuji, sikizani tatongoa. naketele vitongoji, na safari za mashua.  Leo nakumbuka mbiji, ya kutweka na kutua.  Ai,pato na mpewa, litakapo kukutana . Ai, mpewa na pato, lipalo mtu kukuwa. angawa mwana mtoto, wa kutishika kachewa. akiwa na upasito, wa kutamani ukiwa. ai, ndwele na afuwa , itakapokukutana . Ai afua na ndwele, kwa mwenye nayo kutusha. akenda mwendo wa kule, illi kutakawadhisha. aonapo yatumile, akatamani kushasha. ai ,ruhu na maisha itakapo kukutana . Ai ,maisha na ruhu, yamtumupo kiumbe. humshukuru Rabbahu, ni mpambo umpembe. kesho mbele za illahu, swiratwi isimkumbe.  ai, janna na kiumbe itakapo kukutana . Ai,kiumbe na janna,mwanzo asitakiriyo. na kuuza ihisana tumwi ayaghufiriyo. apendalo akaona kwa kila atamaniyo. ai furaha na moyo itakapo kukutana . Ai, moyo na furaha alo n...

MABADILIKO

Hubadili kuwa kovu, kidonda kilopashika, Embe biti huwa bivu, wakaa hubadilika, Wala mwia si mvivu, kwenedakwamba tachoka, Sultani mwenye nguvu, haungoji angataka, Hupita na kupituka
                     KISWAHILI Himdi naabtadi, jinale Jala Jalali, Wa akhiri na wahedi, chanzo cha kila usuli, Tenapo kisha nirudi, nirudi mara ya pili, Nisifu lugha ya jadi, lugha yangu Kiswahili, Tupende lugha faridi, tukipende kiswahili. Lugha ya tangu jadudi, tangu enzi na azali, Tuienzini abadi, tukizingatia ngeli, Tuzishike abjadi, manenoye na methali, Lugha tusiisharidi, tukatukuza za Mbali, Tupende lugha faridi, tukipende Kiswahili. Lugha tuloifanidi, kwa nzuri zake kauli, Mvuto halwaridi, na utamu wa asali, Tuzidi kutia chudi, yenee kila mahali, Kwa zaidi na zaidi, katika zetu shughuli, Tupende lugha faridi, tukipende Kiswahili. Natuifanye fuadi, azizi lugha halili, Tusome tuwe weledi, Kwa ugwiji na unguli, Uwe uvumba na udi, kukuza lugha aali. Nathari iktisadi, zijengwe kitaamuli, Tupende lugha faridi, tukipende Kiswahili. Tupende tuzifaidi, fani zake bulibuli, Tuwape kama zawadi, wageni wa bara ...