HISTORIA YA MUYAKA WA MUHAJI(MUYAKA BIN HAJJ) [1776-1840]

Bw. Muyaka wa Muhaji alizaliwa Mombasa(Mvita,Gongwa,Kongowea,Nyali Kuu,Mzimle.)Mji wa kale ,na aliishi baina ya mwaka wa 1776 na 1840.Alikuwa shaha aliyejulikana sana katika zama zake hadi waleo kwa kutajika kuwa miongoni mwa malenga hodari na mashuhuri maarufu wa Kiswahili.
Bw.Muyaka alifanya shughuli za tijara,akisafirisha malighafi za bidhaa kwa majahazi(mbiji) hadi miji mbalimbali ya ufukwe wa Afrika Mashariki mathalan visiwa vya Ngazija(Comoro islands),Bukini(Malagasy) ,Unguja(Pemba na Zanzibar) na kadhalika.Aidha alisafiri mpaka miji ya Arabuni na Bara Hindi.Mwanamtamba kule hushinda mzee wa kale.Katika kusafiri huku ,Bw.Muyaka aling'amua maarifa mengi ndiposa akawa heshi kuhusishwa mashaurini katika maswala yaliyohusiana na mji wa Gongwa.
Katika aushi yake,Bw.Muyaka alimcha Mterehemezi;hakuwa na makuu na alisikizana na kuelewana na watu wengi.Alipenda kuvalia magwanda makuukuu yaliyoraruka raruraru.Vilevile alikuwa mtu mbaraza aliyependa dhihaka,stihzai,mzaha na utani mwingi.Ithibati ya haya imo katika tungo zake nyingi ambazo maudhui yahusuyo mambo haya yamedhihirika dhahiri shahiri na jahara kama anga takasa isiyo na mawingu mchana wa shamsi la mtikati.

Waaidha,Bw.Muyaka alikuwa jagina na alishiriki katika kondo nyingi zilizopiganwa baina ya Gongwa na miji mingine ya waswahili.Vita hivi vilitokea kwa sababu ya utesi wa mvita na Sayyid Said na uteso wa waswahili wa kisiwa cha 'Amu.Muyaka hakuipendelea kondo ingawa alikuwa wayo.Wakati mmoja mfano, Muyaka alijiunga na kikosi kikubwa cha jeshi la Mvita na Pate kwenda kupigana na jeshi la kisiwa cha 'Amu.Wengine waliokuwa katika jeshi hili ni wamijikenda ambao walikuwa majirani na walioingiliana sana na kuwa na masikizano na Waswahili wa Mvita.Walipofika Lamu walishindwa walishindwa na wengi wao wakakumbwa na mauko(wakafishwa).Kati ya majagina themanini wa Kipate na Wamvita lukuki walifarakana na Sayari ya tatu.
Ndipo wamijikenda wakaasisi msemo wao usemao"Mwenda Pate kauya chuyacho ni chiriro" wakimaanisha kwa Kiswahili"Endaye Pate harudi kirudicho ni kilio"
Bw.Muyaka aling'oa mtunguja mjini kisiwani Gongwa na anakisiwa kuwa alizikwa katika mava/maziara ya Shehe Mvita mahali ambapo pasemekana kuwa ndipo kitovu cha mji wa Mvita,kazkazini mwa kisiwa cha Gongwa.

Comments

Popular posts from this blog