PANDA Panda, panda la mnazi, lanzalo kupapatua Panda, juu ya malazi, moyo wako weshe ngowa Panda,mti wa mapenzi, uwepushie na juwa. Panda ni wako uluwa, panda darajani panda Panda, juu ya farasi, kwa haiba na sitawa Panda, kiwango mkwasi, uukimbie ukiwa Panda, situpe viasi, wendako ukikujuwa Panda ngano na mpunga, afadhali ya viliwa Panda, wimbi wa kimanga, vipawa vya wakupewa Panda usitunde changa, tauwa mbivu tauwa Panda, mwema mshajari, wite tanzu za maua Panda ,utunde johari, mwizi asijezanguwa Panda,juu ya mimbari, ulingane sawasawa. Panda, pandio zi wazi, ukenda kwea nda kwea Panda,kwamba umkwezi, weleweo ni kukwea Panda,wala pasi ngazi shimoni nakungojea Panda,futa na mtama, upate kuvundikia Panda,juu ya mkoma, vijana wakuolea Panda, dua kwa Karima, kwa utakaso na nia.
Comments
Post a Comment