ITAKAPOKUKUTANA
Simba ndume na wambuji,
sikizani tatongoa.
naketele vitongoji, na safari za mashua.
naketele vitongoji, na safari za mashua.
Leo nakumbuka mbiji,
ya kutweka na kutua.
Ai,pato na mpewa,
litakapo kukutana
.
.
Ai, mpewa na pato,
lipalo mtu kukuwa.
angawa mwana mtoto, wa kutishika kachewa.
akiwa na upasito, wa kutamani ukiwa.
ai, ndwele na afuwa , itakapokukutana
.
angawa mwana mtoto, wa kutishika kachewa.
akiwa na upasito, wa kutamani ukiwa.
ai, ndwele na afuwa , itakapokukutana
.
Ai afua na ndwele,
kwa mwenye nayo kutusha.
akenda mwendo wa kule, illi kutakawadhisha.
aonapo yatumile, akatamani kushasha.
ai ,ruhu na maisha itakapo kukutana
.
akenda mwendo wa kule, illi kutakawadhisha.
aonapo yatumile, akatamani kushasha.
ai ,ruhu na maisha itakapo kukutana
.
Ai ,maisha na ruhu,
yamtumupo kiumbe.
humshukuru Rabbahu, ni mpambo umpembe.
kesho mbele za illahu, swiratwi isimkumbe.
humshukuru Rabbahu, ni mpambo umpembe.
kesho mbele za illahu, swiratwi isimkumbe.
ai, janna na kiumbe
itakapo kukutana
.
.
Ai,kiumbe na janna,mwanzo asitakiriyo.
na kuuza ihisana tumwi ayaghufiriyo.
apendalo akaona kwa kila atamaniyo.
ai furaha na moyo itakapo kukutana
.
na kuuza ihisana tumwi ayaghufiriyo.
apendalo akaona kwa kila atamaniyo.
ai furaha na moyo itakapo kukutana
.
Ai, moyo na furaha
alo nayo hunawiri.
na kumuwelea raha apendalo kaamiri.
akiwa mtu maliha, asizagawe ni shari.
ai,udi na ambari itakapo kukutana
.
na kumuwelea raha apendalo kaamiri.
akiwa mtu maliha, asizagawe ni shari.
ai,udi na ambari itakapo kukutana
.
Ai,ambari na udi.
nyoshi za tumwa habibu.
atumiayao abadi, kwandikiwa na thawabu.
tena hunali muradi apendalo likasibu.
ai,fedha na dhahabu, itakapo kukutana
.
atumiayao abadi, kwandikiwa na thawabu.
tena hunali muradi apendalo likasibu.
ai,fedha na dhahabu, itakapo kukutana
.
Ai,dkhahabu na fedha,
vitu vilivyo mfano.
watu hutoa karidha, hapi mwende ile tuno.
watu hutoa karidha, hapi mwende ile tuno.
watoao ni baadha,
wala si kupa hukuno.
ai ,samli na ngano itakapo kukutana.
ai ,samli na ngano itakapo kukutana.
Ai, ngano na samli, viliwa vyema hiyari
Vitu viawavyo mbali, Rena na Baunaghari
Apao mwende akali, Mola humjaza kheri
Ai, ziwa na sukari, vitakapo kukutana.
Ai,sukari na ziwa, litialo mtu kondo
Alo na ndwele hupowa,akapata na mwenendo
Akenda kayikutua, kutambaza nguo pindo
Ai,neno na kitendo, vitakapokukutana
Ai, kitendo na neno, la ahadi na ziasi
Lendeapo siku mno, ni haiba ya upasi
Mwenzo mtake kwa sono, hata awe na nafasi
Ai, simba na farasi,watakapokukutana
Ai,farasi na simba, wangiapo kwenda mbio
Hutarakanya marimba,na kukutakuta nyao
Na kunguruma ja mwamba, ukimbile utishao
Ai, mato na chiyoo, vitakapokukutana
Ai, chiyoo na mato, tia nuru takatifu
Hujaalia jisito, baadaye ukashufu
Ni msabaha wa kito, yaakuti masherafu
Ai, pua na harufu, itakapokukutana.
Ai, harufu na pua, zitatanapo tatizi
Na kiumbe kughumiwa ,lolote asimaizi
Wakati wa kutongowa,zamani za kubarizi.
Ai, mkono na kazi, vitakapokukutana
Ai, kazi na mkono, mtenzi asikuliwe
Ndipo awapo mnono, kajikaga unonowe
Na siku ya makindano, asambiwe hata nawe
Ai, makinda na mwewe, yatakapokukutana
Ai, mwewe na makinda, ayaandikapo mato
Angani hachi kupanda, angawa kinda mtoto
Yuu la anga kutunda, kwa mkono wa kushoto
Ai, godoro na mto,litakapokukutana
Ai, mto na godoro, lipendezalo zitangu
Lenye haiba na duru, na haiba ya kizungu
Alipatalo ni faru, yu katika ulimwengu
Ai, kiti na tawangu, vitakapokukutana
Ai, twangu na kiti, cha ng'amba chenyi zikuku
Kina tumba katikati, na pembe huku na huku
Kinga kitakwi kwa uti,ukipatae hushuku
Ai, chuma na sumaku, vitakapokukutana.
Ai, simaku na chuma, zipambanapo fikira
Muungwana ni hudama, na shujaa huwa bora
Hazipatani kalima, siku ya pia kukara
Ai, dira na duwara, vitakapo kukutana.
Comments
Post a Comment