Posts

Showing posts from January, 2016
                     KISWAHILI Himdi naabtadi, jinale Jala Jalali, Wa akhiri na wahedi, chanzo cha kila usuli, Tenapo kisha nirudi, nirudi mara ya pili, Nisifu lugha ya jadi, lugha yangu Kiswahili, Tupende lugha faridi, tukipende kiswahili. Lugha ya tangu jadudi, tangu enzi na azali, Tuienzini abadi, tukizingatia ngeli, Tuzishike abjadi, manenoye na methali, Lugha tusiisharidi, tukatukuza za Mbali, Tupende lugha faridi, tukipende Kiswahili. Lugha tuloifanidi, kwa nzuri zake kauli, Mvuto halwaridi, na utamu wa asali, Tuzidi kutia chudi, yenee kila mahali, Kwa zaidi na zaidi, katika zetu shughuli, Tupende lugha faridi, tukipende Kiswahili. Natuifanye fuadi, azizi lugha halili, Tusome tuwe weledi, Kwa ugwiji na unguli, Uwe uvumba na udi, kukuza lugha aali. Nathari iktisadi, zijengwe kitaamuli, Tupende lugha faridi, tukipende Kiswahili. Tupende tuzifaidi, fani zake bulibuli, Tuwape kama zawadi, wageni wa bara ...