PANDA
Panda, panda la mnazi, lanzalo kupapatua
Panda, juu ya malazi, moyo wako weshe ngowa
Panda,mti wa mapenzi, uwepushie na juwa.
Panda ni wako uluwa, panda darajani panda
Panda, juu ya farasi, kwa haiba na sitawa
Panda, kiwango mkwasi, uukimbie ukiwa
Panda, situpe viasi, wendako ukikujuwa
Panda ngano na mpunga, afadhali ya viliwa
Panda, wimbi wa kimanga, vipawa vya wakupewa
Panda usitunde changa, tauwa mbivu tauwa
Panda, mwema mshajari, wite tanzu za maua
Panda ,utunde johari, mwizi asijezanguwa
Panda,juu ya mimbari, ulingane sawasawa.
Panda, pandio zi wazi, ukenda kwea nda kwea
Panda,kwamba umkwezi, weleweo ni kukwea
Panda,wala pasi ngazi shimoni nakungojea
Panda,futa na mtama, upate kuvundikia
Panda,juu ya mkoma, vijana wakuolea
Panda, dua kwa Karima, kwa utakaso na nia.
Comments
Post a Comment